______________________________________________________________
______________________________________________________________
Na Yesu akalia tena kwa sauti kuu, akaitoa roho yake.
Ndipo tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka, miamba ikapasuka, makaburi yakafunguka; na miili mingi ya watakatifu waliolala ikafufuliwa; nao wakatoka makaburini baada ya kufufuka kwake, wakaingia katika mji mtakatifu, wakawatokea watu wengi.
Basi yule akida na wale waliokuwa pamoja naye wakimlinda Yesu, walipoona tetemeko la nchi na mambo yaliyotukia, wakaogopa sana, wakisema, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.
(Mathayo 27:50-54)
______________________________________________________________